Utangulizi
Mkataba wa Hudaybiya ulitokana na makubaliano ya amani yaliyowekwa baina ya Mtume Mohammad (rehma na amani zimshukie) na watu wa kabila la Quraysh kutoka Makka, ambao waliwazuia Waislamu takribani elfu moja na mia nne pamoja na Mtume katika eneo lililoitwa Hudaybiya karibu na Makka walipokuwa wakienda Umra. Hivyo ilibidi waingie makubaliano ya amani baina ya pande hizi mbili walifanya mazungumzo na hatimaye walisaini mkataba uliitwa Mkataba wa Hudaybiya
Wasifu wa Mtume Mohammad (rehma na amani zimshukie), unatoa maarifa mengi kuhusu undani wa diplomasia ya kinabii katika kusimamia maswala nyeti ya kufanya maamuzi sahihi ya kisiasa na kukamilisha mazungumzo ya kisiasa kwa weledi na umahiri. Hata hivyo tunaishi katika zama ambazo baadhi ya watafiti wanaonekana kutathmini siasa kwa mtazamo wa fiqhi ya Kiislamu ya zamani inayogawanya jamii katika makundi mawili yaani makafiri dhidi ya Waislamu na Waislamu na makundi haya mawili yametengenezewa mzozo wa milele usiokwisha, pia hukumu zao hutolewa kwa kufuata maandiko kutoka katika vitabu vya siasa za kisheria vilizoandikwa katika kihistoria na kujaribu kuzitumia katika nyakati hizi katika maeneo mbalimbali na sifa kuu ya hukumu hizo ni hudumu kwa muda mrefu na watoaji wa hukumu hizo huwa hawajali kabisa mwingiliano uliopo kati ya maandiko yaliyopita na hali halisi ya sasa.
Katika wasifu wa Mtume tunaona jinsi ambavyo kulikuwa na utofauti wa wazi kati ya muungano wa kisiasa kwa wasio Waislamu na ukweli ni kwamba dola ya Kiislamu haikutambua baadhi ya watu waliodai kuingia katika Uislamu na kudai kuwa wameungana na dola ya Kiislamu haliyakuwa hawafati yale waliyopaswa kufanya. Kutokutambulika huku kulitokana na ukweli kwamba Waislamu hawa wapya hawakufuata uongofu wao kwa kiapo rasmi cha kisiasa kwa dola ya Kiislamu kitu ambacho kwa kawaida ndicho kilichofafanua mahusiano ya kisiasa kati ya pande
mbalimbali na kingewafanya watambulike rasmi kama sehemu ya jamii ya kidini.
Katika utafiti huu tumeangazia misingi kadhaa muhimu ili kuelewa asili ya vitendo vya Mtume na kubainisha rejea zake za msingi zilizonukuliwa kutoka katika wasifu wa Mtume hasa kuhusu tukio moja muhimu la kihistoria: Mkataba wa Hudaybiya Pamoja na usimamizi wa hekima wa mazungumzo yaliyoongoza mkataba huo, mazingira yaliyofuatia katika utekelezaji wa masharti yake, pamoja na uvunjaji wa masharti hayo kwa Maquraysh uliomalizika kwa ushindi wa Makka ambao Quran Tukufu imeutolea sura nzima yaani Surat Al-Fath (Quran: 48).
6. Masomo ya kutumika katika uhusiano wa kimataifa wa sasa
6.1. Muda wa suluhu (Solh): Je, ni suala la muda maalum au la maslahi?
Hudna (mapatano ya kusitisha vita) ni makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda uliowekwa iwe kwa fidia au bila fidia na huitwa muhadana, muwadaa, muahada, musalaha na musalama[1] katika kulielezea hili wanazuoni walitofautiana:
1. Wafuasi wa madhehebu ya Hanafi na Maliki kwa mujibu wa riwaya kutoka kwa Imam Ahmad, wanaamini kuwa hudna inaruhusiwa kwa kipindi ambacho imamu anaona kuwa kuna maslahi hata kama itaizidi miaka kumi. Hii ni kwa sababu kuwa mkataba unaoruhusiwa kwa muda wa miaka kumi, hivyo unaweza kuongezwa kama mkataba wa upangaji na kama faida ya suluhu inaweza kuzidi manufaa ya vita.
2. Mtazamo wa Al-Shafii, unaotokana na riwaya nyingine ya Ahmad unaoeleza kwamba hudna inaruhusiwa kwa miaka kumi tu na haipaswi kuongezwa zaidi ya hapo.
3. Mtazamo wa kwanza ndio unaopewa uzito zaidi: Ibn al-Qayyim alisema, “Inaruhusiwa kufanya amani na watu wa vita kwa ajili ya kusitisha mapigano kwa miaka kumi na pia inaruhusiwa kuongeza zaidi ya hapo kulingana na haja na maslahi yanayotawala.[2]”
Maoni kwamba kipindi cha suluhu hakiwezi kuzidi miaka kumi ni dhaifu. Tunaweza kuanzisha hali ya amani duniani kwa msingi wa mapatano na mikataba ya amani katika makubaliano ya kimataifa ambayo huanzisha uhusiano wa amani kupitia mikataba inayotoa hadhi ya kudumu.
6.2. Tofauti kati ya mkataba wa kisiasa na mkataba wa kiimani Umuhimu wa kutekeleza mikataba ni moja ya maadili muhimu zaidi ya kisiasa na kimaadili katika Uislamu kwa sababu huwezesha kuzaliwa kwa dola ya Kislamu ambayo ndani yake huanziashwa taasisi ya mkataba wa kisiasa wa hiari kati ya pande zinazoshirikiana katika dola hiyo. Hili halitokani na itikadi kama baadhi ya harakati za Kiislamu zinavyodhaniwa wala si zao la utawala wa mabavu au kulazimisha.
Mara kwa mara watu wengi huchanganya kati ya masuala ya uaminifu na kujitenga (alWalaa
wal Baraa) kwa kuchanganya mkataba wa kisiasa wa dola ya Kiislamu pamoja na mkataba wa kiimani wa umma wa Kiislamu na kuzichukulia mikataba hiyo miwili kuwa kitu kimoja.
Hali halisi ni kwamba kuingia katika mkataba wa kiimani na Waislamu kama jamii na akida haimaanishi kuwa mtu huyo ameingia pia katika mkataba wa kisiasa kimyakimya au moja kwa moja na dola ya Kiislamu kama sharti la lazima na lisilotenganika.
Mkataba wa kiimani unamaanisha kwamba mtu huyo ameukubali Uislamu kama dini na kushikamana na wajibu na majukumu yake. Hii haimlazimishi kuingia katika mkataba wa kisiasa kama raia chini ya dola hiyo au kuitii mamlaka yake.
Na mkataba wa kiimani haumlazimishi mtu kujiunga kisiasa na jamii ya Kiislamu ili imani yake iwe sahihi na kamilifu kwa kuwa watu wengi wanaweza kuingia katika mkataba wa kiimani wakiwa nje ya mipaka ya kijiografia ya Dola ya Kiislamu.
Ifahamike kuwa mkataba wa kisiasa ni makubaliano ya kuishi ndani ya dola ya Kiislamu kwa kuitii sheria zake na kushiriki katika vita na amani kupitia mikataba ya ulinzi wa pamoja hujumuisha uhifadhi na uangalizi wa kisiasa wa dola hiyo. Na mtu anayefanya mkataba huu anaweza kabisa asiwe Muislamu au huenda hajawahi kabisa kuingia katika mkataba wa kiimani. Hii haimzuii yeye kuingia katika mkataba wa kisiasa kwa kuwa wasio Waislamu wengi wanaweza kuwa sehemu ya muundo wa Dola ya Kiislamu na kuishi ndani ya mipaka yake bila kushikamana na Uislamu hata kidogo.
Maana hii inadhihirika wazi katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na wale waliomuamini lakini hawakuhama, basi nyinyi hamna ulinzi juu yao mpaka wahame. Na wakikuombeni msaada kwa ajili ya dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipokuwa dhidi ya watu ambao baina yenu na wao kuna mkataba. Na Mwenyezi Mungu anaona mnayoyatenda.” (Qur’an 8:72)
Hivyo basi tunaona kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu haikuitaja hijra kama tendo la lazima, bali kama ishara ya kuingia katika mkataba wa kisiasa wa dola. Na kutokuhama hakubatilishi hukumu ya Uislamu na imani.
Katika tafsiri yake, Sheikh Al-Saadi alitoa maana ya wazi kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na wakikuombeni msaada kwa ajili ya dini,” yaani: ikiwa watu wa Imani (Waislamu) wataomba msaada kwa sababu wanashambuliwa kwa ajili ya dini yao, “basi ni juu yenu kuwasaidia,” yaani: kuwasaidia kwa kupigana pamoja nao. Lakini kama walishambuliwa kwa sababu nyingine, kama kuendeleza uadui, kufanya dhuluma na maovu mengine basi Waislamu hao hawapaswi kusaidiwa.[3]
Kupitia maana hizi, tunaona kwamba Qur’ani inaweka msingi imara wa kutenganisha kati ya masharti ya mkataba wa kiimani na masharti ya mkataba wa kisiasa. Jambo hili lilionekana kwa vitendo katika mwenendo wa kisiasa wa Mtume (ﷺ) siku ya Hudaybiya. Miongoni mwa masharti yaliyowekwa katika suluhu hiyo, tunataja vipengele viwili:
1. Kipengele cha Kwanza:
“Kurejeshwa kwa kila mtu atakayekwenda kwa Waislamu (kambi ya Mtume huko Madina) kutoka kwa Maquraish akiwa Muislamu bila ruhusa ya Maquraish, lakini Maquraish hawatalazimika kuwarudisha Waislamu watakaowarudia wao (huko Makka) kama wameasi Uislamu.”
Baada ya mkataba kuandikwa, Abu Jandal bin Suhail bin Amr alifika akiwa amefungwa minyororo, akikimbia kutoka kwa washirikina wa Makka. Mtume (ﷺ) alimrudisha kwa washirikina kwa mujibu wa masharti ya mkataba, jambo lililomfanya Abu Jandal kusema:
“Enyi Waislamu je, nitarudishwa kwa washirikina ili wanitie fitinani katika dini yangu?!” Mtume (ﷺ) akamwambia: “Tumeweka ahadi kati yetu na wao na hatutaivunja.” Katika muktadha huu ni dhahiri kwamba Abu Jandal hakuwa amejiunga na mkataba wa kisiasa pamoja na Waislamu, kutokana na uaminifu wa Mtume (ﷺ) kwa masharti ya Mkataba wa Hudaybiya. Hata hivyo, hilo halikubatilisha kuwa kwake Muislamu wala uhusiano wake wa kiimani na Mungu na Mtume wake.
2. Kipengele cha Pili:
Uhuru kwa mtu au kabila lolote kuingia katika mkataba wa Quraysh au ule wa Mtume. Hapa ndipo kabila la Banu Khuza’ah liliposimama na kusema: “Sisi tupo katika mkataba wa Muhammad,” na Banu Bakr wakasema: “Sisi tupo katika mkataba wa Quraysh.”Wengi wa Banu Khuza’ah walikuwa bado wanaabudu masanamu na walikuwa makafiri.
Hili ni uthibitisho mwingine kutoka katika maisha ya Mtume (ﷺ) unaoonyesha kwamba mkataba wa kisiasa ulitenganishwa kabisa na mkataba wa kiimani. Kwa mara nyingine tena kabila la Khuza’ah lilikuwa bado limeghubikwa na ushirikina na kutokuamini. Hawa waliweza kuingia katika mkataba wa kisiasa wa utii na ulinzi na Mtume, japokuwa hawakuwa Waislamu wala wakaazi wa Madina. Hili halikuwazuia kuingia katika mkataba wa kisiasa wa kuungwa mkono iwapo wangetendewa uadui.[4]
Wakati huo huo Abu Jandal ambaye alikuwa ndani ya Uislamu na ana imani ya dhati, alikatazwa kuingia katika mkataba huo wa kisiasa kwa mujibu wa masharti ya Mkataba wa Hudaybiya.
Ahadi ya Pili ya Aqaba:
Ahadi ya pili ya utii ilikuwa kati ya Mtume na Ansar ilihusisha vipengele vya mkataba wa kisiasa, na ilikuwa ahadi ya kisiasa kwa kiwango kikubwa, ilhali ahadi ya kwanza ilikuwa ni ya kiimani tu.
Katika maandishi ya ahadi ya pili ya Aqaba, Ansar walimuuliza Mtume: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tutakuahidi nini?” Akasema: “Niahidini kwa kusikiliza na kutii wakati wa hamu na kuchoshwa katika hali ya matumizi, wakati wa shida na raha, kwa kuamrisha mema na kukataza maovu, kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, msihofu lawama ya wenye kulaumu, na kwamba mtaanza kunisaidia iwapo Yathrib itanishambulia; mchukie mbali nami kile mnachokichukia mbali na nafsi zenu, wake zenu na watoto wenu na Pepo ni yenu.”[5]
Katika mkataba huu wa imani na siasa, inakuwa dhahiri kwamba ulinzi na msaada unapaswa kutolewa ikiwa tu Mtume atahama kwenda kwao na hapo ndipo wangemlinda ndani ya Yathrib tu.
Muhtasari wake unaonyesha jinsi Mtume (ﷺ) alivyotofautisha wazi kati ya uhusiano wa kiimani na wa kisiasa na jinsi alivyotenda kwa misingi hiyo katika mkataba wa Hudaybiya na ahadi za Aqaba.
Hiyo ndiyo sababu tunamkuta Mtume (ﷺ) siku ya Badr hakuchukua hatua ya vita nje ya Madina bila idhini ya Ansar. Alisema siku hiyo: “Nishaurini, enyi watu.”
Maswahaba kadhaa walisimama na kutoa maoni mazuri. Kisha Sa’d bin Mu’adh, kiongozi wa Ansar, akasimama na kusema:
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kana kwamba unatuashiria sisi, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Mtume akasema: “Ndiyo.”
Sa’d akasema:
“Tumeamini kwako, tumekuamini, tumeshuhudia kwamba ulichokuja nacho ni kweli, na tumekupa ahadi na mikataba yetu ya kusikiliza na kutii. Haya, nenda Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu utakavyo, kwani tupo pamoja nawe. Naapa kwa Yule aliyekutuma kwa haki, lau ungelituonyesha bahari na ukaingia ndani yake, tungeingia pamoja nawe wala hakuna hata mmoja wetu atakayebaki nyuma. Hatuchukii kukutana na adui yetu kesho. Sisi ni wavumilivu vitani, waaminifu tunapokutana na Mwenyezi Mungu atakuonyesha kutoka kwetu yale yatakayokufurahisha macho yako. Basi tembea pamoja nasi kwa baraka za Mwenyezi Mungu.”
Hivyo basi, tunaona wazi kuwa Mtume (ﷺ) hakuwalazimisha Ansar kupigana katika vita vya Badr vilivyofanyika nje ya mipaka ya Madina, isipokuwa baada ya kupata idhini kutoka kwao. Hakuwa ameenda kinyume na masharti ya mkataba wa kisiasa uliowekwa katika Ahadi ya Pili ya Aqaba kati yake na Ansar ingawa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na utiifu kwake ni wajibu.[6]
Hili linatufikisha katika uhitaji wa kutafakari kwa kina juu ya utofautishaji kati ya mkataba wa kisiasa na mkataba wa kiimani katika maudhui yao, athari zao na haki na wajibu wa kila mmoja. Ni muhimu kutowachanganya au kuwaleta kama kitu kimoja au kudhani kwamba masharti ya mmoja ni lazima yawe ya mwingine, kiasi kwamba mtu akijiondoa kwenye mmoja basi na mwingine unaathirika.
Kwa hiyo lazima kutofautisha kati ya uaminifu wa imani (al-wala’) na uaminifu wa kisiasa, vivyo hivyo kati ya kujitenga kwa kidini na kujitenga kwa kisiasa, jambo ambalo limechanganywa sana na makundi mengi ya Kiislamu.
Tunarejea pia kwenye suala muhimu na nyeti sana:
Sheria ya upanga na mamlaka, hata kama huleta dola kama taasisi ya kiserikali, haipati uhalali wake isipokuwa kupitia mkataba wa kisiasa wa makubaliano ya hiari kati yavipengele mbalimbali vya jamii chini ya mfumo wa mamlaka ya eneo la nchi hiyo.
6.3. Kanuni katika uhusiano wa kimataifa na uhifadhi wa maagano na mikataba pale inapopinga matawi ya Sheria za Kiislamu
Ni muhimu kuwa na utulivu wa kisiasa kwa kudumisha makubaliano ya mikataba waliyoingia kwa gharama ya utekelezaji wa matawi ya sheria, kwani kutekeleza maaagano na makubaliano hayo ya mikataba ndio msingi wa kisheria. Tunapata nukuu hizi katika sera ya Nabii aliyerudi kutoka Hudaybiya kwenda Medina alisema Abu Basir mwanamume Mwislamu kutoka Quraysh alimfikia, hivyo walitumwa wanaume wawili kutoka Quraysh kumtafuta mtu huyo na wakasema: “Likumbuke agano ulilofanya nasi.” Basi, akapelekwa kwa wanaume hao na wakaondoka naye na walipofika katika kikosi cha washirika walikaa na kula tende kutoka kwao. Abu Basir akamwambia mmoja wa wanaume: “Naamini kwa Mwenyezi Mungu naona upanga wako vizuri sana ewe ndugu,” yule mwingine akautoa na kusema: “Ndio hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri nimeujaribu
kisha nikaujaribu tena.” Abu Basir akasema: “Nionyeshe nipate kuuangalia.” aliopompatia akamshika na kumpiga nao hadi akafa na yule mwingine akakimbia hadi akafika Medina na akakimbilia msikitini. Ndipo Nabii alipomwona akasema: “Huyu mtu ameona jambo la kutisha.” Alipomfikia Nabii, akasema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwenzangu ameuawa na mimi nitauliwa.” Kisha Abu Basir akaja na kusema: “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amekamilisha wajibu wako, umenirudisha kwao, kisha Mwenyezi Mungu aliniponya kutoka kwao.” Nabii akasema “Ole wake mama yake, mchochezi wa vita, kama angalikuwa na mtu.”
Kauli ya Nabii, “Ole wake mama yake,” ni neno la kejeli ambalo Waarabu husema kwa sifa, wala hawamaanishi maana ya kejeli ndani yake. Na kauli yake: “mchochezi wa vita” inamaanisha kuwasha moto wa vita kwa sababu ya alichofanya kwa kumuua yule mtu. Na kauli yake: “Kama angalikuwa na mtu,” yaani, kumuunga mkono, kumsaidia au kumwokoa. Na humo kuna ishara kwenda kwake kukimbia ili asirudishwe kwa washirika ni alama kwa yeyote kati ya Waislamu wanyonge huko Mecca aliyepata habari hii, ajiunge naye. Abu Basir aliposikia hilo, alijua kuwa atarudishwa kwao, kwa hivyo akatoka hadi akafika pwani. Akasema: Abu Jandal bin Suhail alikimbia kwao kwa hivyo akajiunga naye na akafanya hivi kwamba hakuna mwanamume yeyote kutoka kwa Quraysh aliyeingia Uislamu pasipo kukutana na Abu Basir na wangekaa hadi kuunda kundi kubwa na pale waliposikia ngamia yoyote iliyotoka kwa Quraysh kwenda Syria waliiteka
wakauwa na kuchukua mali zao [7]
7. Hitimisho
Mkataba wa Hudaybiya ulikuwa ushindi wa kisiasa wenye maana na ulivuna mavuno mengi zaidi ya mbegu yake, kwa sababu ya msaada wa Mungu, hekima ya kisiasa na maono ya kimkakati ambayo Nabii alikuwa akiyaangalia katika upeo wa mustakabali wa mbali. Faida hizi ni jumla ya mafanikio ya kimkakati, ambayo hayawezi kamwe kulinganishwa.
7.1. Kupata kutambuliwa kisiasa kutoka kwa Quraysh
Kabla ya Mkataba wa Hudaybiya, Quraysh walisisitiza kuangamiza Waislamu kwa ajili hii walipigana vita vitatu katika Badr na moja katika Khandaq lakini wakashindwa kuwaangamiza. Leo hii Waislamu wanakaa pamoja na Quraysh na kuandika mikataba nao na hii ni dalili muhimu ya umuhimu wa kupata utambulisho wa kimataifa kwa serikali ambayo Waislamu wanataka kuanzisha. Vinginevyo itageuzwa kuwa serikali iliyotengwa na ulimwengu.
7.2. Umuhimu wa usalama wa kudumu na uhuru wa shughuli za da’wa ya Kiislamu (kazi ya kueneza ujumbe wa kidini) Mkataba wa Hudaybiya ulithibitisha kwamba Uislamu unapata zaidi katika mazingira ya utulivu kuliko katika mazingira ya vita. Mkataba wa Hudaybiya ulikuwa ushindi, kama Mwenyezi Mungu alivyouita katika Surah al-Nasr na kama mafanikio katika Surah AlFatiha.
Na ushindi hapa ni mafanikio ya da’wa na kuingia kwa watu katika dini ya Mwenyezi Mungu, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: “Mwisho wa ushindi wa Mwenyezi Mungu na mafanikio yamekuja, na unaona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa wingi.” (Qur’an, 110:1-2). Watu wengi walijiunga na Uislamu katika hatua hii, na inatosha kujua kwamba idadi ya Waislamu wakati wa Mkataba wa Hudaybiya ilikuwa takriban 1,400, na waliposhinda Makka 10,000 waliingia. Miongoni mwa wale waliojiunga na Uislamu wakati wa Hudaybiya na ushindi wa Makka walikuwa Khalid ibn Al-Walid na Amr ibn Al-Aas. Hii ni dalili msingi ya umuhimu wa usalama wa kudumu na kufikia hali ya mawasiliano na uhuru wa kufikia malengo ya da’wa katika uenezaji, ambayo haipatikani kamwe katika hali ya vita na mapigano. Hii ndiyo Waislamu wanapaswa kuitafuta katika enzi hii ya kuimarisha uhusiano na watu wa ulimwengu na kujenga msingi wa amani unaoleta utulivu na uhuru.
7.3. Kuhamia kutoka ngazi ya ndani hadi kimataifa
Katika hatua hii ambayo amani na utulivu vilipatikana, Nabii alitumia fursa hiyo kuandikia wafalme wa ulimwengu kwa hivyo, aliandikia Heraclius, kiongozi mkuu wa Warumi; Khosrau kiongozi wa Wajemusi; Al-Muqawqis kiongozi wa Wakopti na viongozi wengine wa kimataifa. Mazungumzo yalianza kwa mwaliko wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa wafalme hao kuingia katika Uislamu. Hii ni dalili muhimu ya mwingiliano na mazingira ya kimataifa, badala ya kujifunga katika mipaka ya ndani na kujitenga na ulimwengu.
7.4. Waislamu kuwa nguvu isiyoweza kupuuzwa Hii inaonekana katika mambo mawili:
1. Mwelekeo wa wanasiasa wenye hekima wa Quraysh – Waliunga mkono mwelekeo wa amani na kama wangalikuwa na nguvu na uwezo wa kutosha, wangalichagua vita na mivurugo.
Ushiriki wa kabila la Khuza’a katika muungano wa Kiislamu – Khuza’a hawakuwa Waislamu wakati huo, lakini waliingia kwenye mkataba kwa hiari yao. Unganisho muhimu: Mwanasiasa mwenye ujuzi huelekea kufungua njia za mawasiliano na mazungumzo wakati ana nguvu na uwezo wa kutosha, akimpa mpinzani wake fursa ya kuelekea kwenye amani. Mwanasiasa hodari sio yule anayepindukia amani tu wakati ameshindwa na huchagua mazungumzo kama njia ya kujisalimisha.
Hitimisho la Ujumla
Mkataba wa Hudaybiya ulikuwa mchakato wa kimkakati ulioleta mafanikio makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kidini. Ulifungua milango ya kuingia kwa Uislamu kwenye ngazi ya kimataifa, kuimarisha nafasi ya Waislamu kama nguvu ya kukubalika na kuweka msingi wa amani ya kudumu ambayo iliruhusu uenezaji wa da’wa kwa uhuru. Mafundisho ya mkataba huu yana umuhimu mkubwa kwa Waislamu wa leo katika kujenga uhusiano na ulimwengu kwa hekima, uvumilivu na mipango ya baadae.
[1] [1] Jurisprudence Explained: (7/243) Dr. Abdullah bin Muhammad Al-Tayyar, Dr. Abdullah bin Mohammed Al-Mutlaq, Dr. Mohammed bin Ibrahim Al Musa. Publisher: Madar Al-Watan Publishing, Riyadh: Volumes 7, 11–13; 1st edition: 1432/2011
[2] Elucidation of the Rulings of ibn Bassam (Vol. 6).
[3] Interpretation of Sheikh Al-Saadi (Vol.1, p.196) Researcher: Abdul Rahman bin Mualla Al-Luhaiq. Publisher: Al-Risaala Foundation. 1st Edition: 1420 AH / 2000 AD.
[4] For details see Zad Al-Ma’ad (Vol. 3 / pp. 255–262) Publisher: Al-Risaala Foundation, Beirut. Al-Manar Islamic Library, Kuwait.
[5] Al-Sunan Al-Kubra lil-Bayhaqi [=Al-Sunan al-Kabir] (17735) Researcher: Muhammad Abdul-Qadir Atta Publisher: Dar Al-Kutub Al-Ilmiyya, Beirut – Lebanon. 3rd Edition: 1424 AH / 2003 AD.
[6] Evidence of Prophecy by Al-Bayhaqi (vol. 3 / p. 34) Publisher: Dar Al-Kutub Al-Ilmiyya – Beirut; 1st Edition 1405 AH.
[7] Narrated by Al-Bukhari Hadith No. (2731, 2732), Book: Conditions, Chapter: Conditions in Jihad and Reconciliation with People of War and Writing Stipulations. Researcher: Muhammad Zuhair bin Nasser Al-Nasser, Publisher: Dar Touq Al-Najat (Illustrated by the Sultanate, adding the numbering of Muhammad Fouad Abdul-Baqi) 1st Edition: 1422 AH.